Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ustadh Sayyid Muhammad Husseini Qazwini, katika kozi maalum na kikao cha kielimu cha “Utafiti wa Fatwimiyya” kilichofanyika Jumamosi katika Hawza ya Hujjat Wali al-Asr (a.t.f.s) katika eneo la Pardisan, Qom Iran, alieleza kuwa: Kuna zaidi ya riwaya 40 zinazoonesha kwamba watu wengi walikuja kumposa Bibi Fatima mtakatifu (a.s), lakini Mtume (s.a.w.w) alisema: “Jambo la ndoa ya Fatima (a.s) liko mikononi mwa Mwenyezi Mungu.” Ndoa ya Ali (a.s) na Fatima (a.s) Iliamuliwa na Mwenyezi Mungu
Rais wa Taasisi aliongeza kuwa Mtume (s.a.w.w) alitangaza juu ya mimbari kwamba kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ndoa ya Bibi Zahra (a.s) na Imam Ali (a.s) ilifungwa katika ulimwengu wa Mtukufu; kama alivyosema:
«ما زوجتُها ولکنّ الله زوّجها فوقَ عرشِه»
“Sikumwozesha mimi, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyemwozesha juu ya Arshi yake.”
Riwaya hii pia imenukuliwa katika vyanzo vya Ahlus-Sunna.
Umuhimu wa Kurejea Katika Vyanzo vya Ahlus-Sunna kwa Ajili ya Hoja, Sio Historia
Ustadh Husseini Qazwini alisisitiza kuwa vyanzo vya Ahlus-Sunna si marejeo ya uandishi wa historia ya Kishia. Alifafanua: Hatutegemei vitabu vyao kuandika historia ya Uislamu, lakini tunavirejea kwa ajili ya kuthibitisha hoja na uhalali wa madhehebu yetu.
Mwalimu huyu wa Hawza ya Qom akirejea Qur’ani Tukufu, Aya ya 93 ya Suratu Aali-Imran, alisema: Mtume (s.a.w.w) aliwaambia Mayahudi:
«قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِنْ کُنْتُمْ صَادِقِینَ»“Sema: Leteni Taurati na muisome ikiwa mnasema kweli.”
Njia hii ya Qur’ani inatufundisha kuwa katika mijadala ya itikadi, kurejea katika vyanzo vya upande wa pili si kosa. Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s) pia walifanya hivyo mara nyingi.
Kurejea Katika Sahih Bukhari na Muslim Kuhusu namna ya Udhu
Ustadh Husseini Qazwini aliendelea kueleza baadhi ya riwaya za Ahlus-Sunna kuhusu namna sahihi ya kuchikua wudhu na akasema: Katika Sahih Bukhari (toleo la Saudi), zipo riwaya kadhaa ambazo Abdullah bin Umar anasimulia: Tulikuwa kwenye safari na Mtume (s.a.w.w), na tulipokuwa tukichukua wudhu, “فجعلنا نمسح علی أرجلنا” yaani: tulikuwa tunapaka juu ya miguu yetu.
Kauli hii inaonesha wazi kuwa katika kuchukua udhu kulikuwa na kupaka miguu, sio kuosha. Hadithi hii inapatikana katika sehemu kadhaa za Bukhari na pia katika Sahih Muslim hadithi namba 241.
Ustadh akasema: Ikiwa kupaka miguu ni batili, je, maswahaba walikuwa wakifanya wudhu batili mbele ya Mtume (s.a.w.w)?!
Kuthibitisha Wilaya ya Imam Ali (a.s) Kupitia Vyanzo vya Ahlus-Sunna
Rais wa Taasisi ya Utafiti aliongeza kuwa; katika masuala kama ukhalifa wa Imam Ali (a.s), tunategemea Ayah na hadithi zilizothibitishwa katika vyanzo vyao. Kwa mfano, katika Aya:
“Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu…”
wanazuoni wakubwa kama Tabari, Ibn Abi Hatim na Alusi wamethibitisha kuwa Aya hii iliteremshwa kuhusu wilaya ya Ali (a.s).
Aidha, katika tukio la Aya ya Ufikishaji, Aya ya Ukamilifu wa Dini, na Hadithi ya Ghadir, kurejea katika vyanzo vya Ahlus-Sunna ni njia ya kielimu na yenye nguvu ya kubainisha haki ya Shia, na hii ni sawa kabisa na mbinu ya Qur’ani na Sunna ya Ahlul-Bayt (a.s).
Riwaya Kuhusiana na Shahada ya Bibi Fatima Zahra (a.s)
Ustadh Husseini Qazwini aliendelea kusema kuhusu shahada ya Bibi Fatima Zahra (a.s): Marehemu Sheikh Kuleyni amenukuu kwa sanad sahihi kutoka kwa Imam Musa al-Kadhim (a.s), ambapo Muhammad bin Yahya anasimulia kutoka kwa Imam (a.s) kuwa amesema:
«ان فاطمه صدیقه الشهیده»“Hakika Fatima ni mkweli na shahidi.”
Je, tunahitaji kauli iliyo wazi zaidi ya hii kuthibitisha shahada yake?
Aliongeza kuwa riwaya nyingine na ushahidi mwingi umeelezwa kuhusu shahada ya Bibi Zahra (a.s). Allamah Majlisi katika Mir’āt al-‘Uqūl amenukuu kuwa riwaya ya shahada ya Bibi Zahra (a.s) ni sahihi.
Vilevile, Marhum Ayatullah al-Khui na Marhum Ayatullah Sheikh Jawad Tabrizi wote wamesema kwa sanad thabiti kutoka kwa Imam Kadhim (a.s) kwamba Bibi Zahra alikuwa: «مظلومة الشهیده» aliyedhulumiwa na shahidi.
Hadhi ya Bibi Zahra (a.s) Katika Vitabu vya Ahlus-Sunna
Mwalimu wa Hawza alisema: Miongoni mwa hadithi nyingi zilizopo katika vitabu visivyo vya Kishia kuhusu hadhi ya Bibi Zahra (a.s) ni hadithi ya Mtume (s.a.w.w) katika Sahih Bukhari, Juzuu ya 4, uk. 209, hadithi namba 3711, ambapo Mtume amesema:
«فاطمة سیدة نساء اهل الجنة»“Fatima ni bibi wa wanawake wa peponi.”
Rais wa Taasisi aliongeza kuwa katika kitabu hicho hicho, Juzuu ya 4, uk. 210, hadithi 3714, Mtume (s.a.w.w) amesema:
«فمن أغضبها فقد أغضبنی»“Yeyote atakayemkasirisha (Fatima), basi amenikasirisha mimi.”
Maoni yako